Wakala Nami ni mfumo unaowaunganisha Wakala Wakuu na Wakala Wadogo ili kurahisisha usimamizi wa float na ufuatiliaji wa miamala kwa haraka, usalama na ufanisi.
Wakala nami inakupatia huduma mbali mbali kutokana na shughuli za uwakala. Zikiwemo:
Pata float kwa urahisi na uhakika kutoka kwa mawakala walio kwenye mtandao wako kwa urahisi na haraka.
Mfumo unaonyesha kwa uwazi fedha zinazoingia na kutoka ili wakala aweze kujua hali yake ya kifedha wakati wote.
Hifadhi taarifa za miamala na maombi ya float. Fuatilia taarifa kwa urahisi na haraka kwa kupata ripoti ya muda husika.
Mfumo unatengeneza ripoti mbalimbali za kifedha na utendaji ili kusaidia kufanya maamuzi ya kibiashara.
Mfumo unaonyesha taarifa na mabadiliko yote kwa muda halisi, hivyo maamuzi yanafanyika kwa haraka na kwa usahihi.
Kila wakala anahakikiwa na kulindwa kupitia hatua za usalama zinazozuia udanganyifu na matumizi mabaya.
Wakala nami inakupa faida na kusaidia katika shughuli mbali mbali za mzunguko wa fedha.
Programu ya Wakala Nami inakuletea kila dashibodi, ombi la float, na taarifa za miamala mahali popote ulipo.
Wasiliana nasi kwa maswali, maombi ya huduma, au usaidizi wowote unaohitaji katika shughuli zako za uwakala.